Bruno Mars Avunja Rekodi Yake Mwenyewe Spotify

Bruno Mars ameendelea kuvunja rekodi kwenye Spotify, akiwa msanii wa kwanza wa kiume kufikia wasikilizaji milioni 150 kwa mwezi. Hii inazidi hatua zake za mwanzo, alipoifikisha wasikilizaji milioni 140 na 130.

Kolabo yake na #SexyyRed kwenye wimbo “Fat Juicy and Wet” umechochea umaarufu wake. Mafanikio ya wimbo huu, pamoja na mkusanyiko wa nyimbo zake maarufu, yamemfikisha kwenye hatua hii ya kihistoria.

Bruno Mars Anaendelea Kuwa mwenye nguvu kubwa kwenye biashara ya muziki, akithibitisha kuwa muziki wake unapendwa na kufurahiwa na mamilioni ya watu duniani .