Burna Boy Anasema Kuwa Ku-Copy Nyimbo Ni Njia Ya Kutoa Heshima .

Burna Boy kwenye Mahojiano Na Jarida La Billboard France Amejibu Suala La Ku-Sample (Copy) Ngoma Za Mastaa Kama Tony Braxton, Brandy, Jeremih N.k, Akidai Kuwa Ku-Sample Ngoma Ni Moja Ya Njia Ya Kutoa Heshima Kwa Waliokushawishi/ Kwa Miziki Iliyomjenga .

Burna Boy Akijibu Suala Hilo La Ku-Copy Kama Alifanya Kusudi; –

“Ndio Nilipanga Kufanya Hivo. Kwani Ku-Sample Ni Nijia Ya Kutoa Heshima Kwa Muziki Ambao Umenitengeneza Mimi. Ni Kuhusu Kuziunganisha Tamaduni Na Kuonesha Kuwa Muziki Ni Lugha Ya Dunia. Nitaendelea Kufanya Hivyo Kwasababu Ukuaji Kimuziki Na Ubunifu Ni Vitu Vinavyokwenda Sambamba” – Burna Akiweka Wazi Kuwa Ataendelea Kufanya Sampling Ya Ngoma Za Mastaa Wakubwa/ Zamani.

Kumbuka Moja Ya Wimbo Ambao Burna Boy Ali-Copy Ni “Last Last” Uliopo Kwenye Album Yake Ya “I Told Them”. Burna Boy Ali-Copy Ngoma Hii Kutoka Kwenye Wimbo Wa Mkongwe Wa Muziki Wa Marekani Tony Braxton Uitwao “He Was A Man Enough”. Huku Akiweka Wazi Kuwa Braxton Anapata Asilimia 60 Ya Mapato Yatokanayo Na Wimbo Huo.

Kwasasa Burna Boy Anatarajia Kuachia Album Yake Mpya “No Sign Of Weakness”.