CHADEMA yakosa Sifa kushiriki Uchaguzi Mkuu 2025

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Ramadhani Kailima amesema kuwa Chama ambacho hakikusaini kanuni za maadili ya uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani wa mwaka 2025 leo Aprili 12, 2025 hakitashiri uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu na chaguzi zote ndogo zitakazofuata kwa muda wa miaka mitano.

Kailima ametoa ufafanuzi huo baada ya vyama 18 Kati ya 19 vyenye usajili wa kudumu kusaini kanuni hizo Katika ofisi ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Kailima amesema vyama vyote vilipewa taarifa kwa maandishi na kwa kupigiwa simu na wote walipokea taarifa ya tukio hilo.

Mapema leo Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika, alitangaza kutoshiriki kwenye kikao cha kusaini Kanuni ya Maadili ya Uchaguzi kwa mwaka 2025, na kueleza kuwa yeye ndiye mwenye mamlaka ya kisheria kusaini kwa niaba ya chama, na hajamteua kiongozi au afisa yeyote kuwakilisha CHADEMA kwenye kikao hicho.