Chris Brown ashitakiwa kwa kumshambulia mtu kwenye klabu ya Usiku

Chris Brown Ameripotiwa Kukamatwa Akiwa Hotelini Jijini Manchester, Nchini Uingereza Baada Ya Maafisa Usalama Wa ‘Met’ Kubaini Kuwa Muimbaji Huyo Ametua Jijini Humo Kwa Ndege Binafsi (Private Jet).

Kukamatwa Kwake Ni Kufuatia Msala Alioufanya 2023 Nchini Humo Wa Kumpiga Na Chupa Ya Mvinyo Producer Wa London Aitwaye ‘Abe Diaw’ Hadi Kuzimia.

Chris Brown Hadi Sasa Yupo Kituo Cha Polisi Kwa Ajili Ya Mahojiano. Kumbuka Pia Mtayarishaji Huyo Alimfungulia Kesi Breezy Akidai Fidia Ya $16M (Tsh Bilioni 43.1/=) Kwa Kumsababishia Majeraha Na Hasara.