Mashabiki wa muziki barani Afrika na duniani kote wamepata matumaini ya ujio wa kolabo kati ya nyota wa Marekani @ciara 🇺🇸 na SIMBA 🦁 @diamondplatnumz. Hii inakuja baada ya #Ciara kuonekana akitumbuiza huku sauti ya Diamond ikisikika kwenye show hiyo Wakati Akiwa Kwenye Ziara Yake.. jambo lililoibua tetesi za kazi kati Ya wawili hao.
Ciara ni mmoja wa wasanii wa R&B Na Pop wenye ushawishi mkubwa duniani Akiwa Ameshinda Tuzo Nyingi Zaidi ikiwemo Grammy, Billboard Music Awards na MTV Video Music Awards. Pia amewahi kuwa Kinara kwenye chati za dunia kupitia nyimbo maarufu kama “How We Roll Ft Chris Brown”, “Goodies”, “1, 2 Step” na “Level Up”.
Nyota huyo anatarajia kuachia album yake mpya “Cici” tarehe 22 Agosti 2025, na mashabiki wanasubiri kwa hamu kuona kama jina la Diamond litajitokeza kwenye orodha (Tracklist) ya nyimbo hizo.
Got a Questions?
Find us on Socials or Contact us and we’ll get back to you as soon as possible.