CPA. Makalla awapa mkono wa heri Makonda na Gambo arusha mjini “Wote wadogo zangu”

Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, CPA. Amos Makalla amewatakia kila la heri Mkuu wa Mkoa wa Arusha wa Sasa, Paul Makonda pamoja na Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Mrisho Gambo, akisema kuwa wote ni watoto wa baba na Mama mmoja ambaye ni CCM.

CPA. Makalla ametoa Baraka hizo leo Juni 06, 2025 wakati akizungumza na Wananchi wa Arusha, ikiwa ni muendelezo wa Ziara yake kwenye mikoa ya Kaskazini, ikiwemo Manyara na Kilimanjaro.

Akizungumzia na Wananchi wa Arusha kwenye mkutano huo CPA. Makalla amesema Makada hao wa CCM wote ni Marafiki na Wanatoka kwenye Familia moja ya Chama cha Mapinduzi, huku akiweka wazi kuwa wanachopitia kwa sasa ni kipindi cha mpito na watakaa sawa kikipita.