Derby ya Kariakoo kupigwa ufunguzi wa pazia la Ligi Kuu 2025/26

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limetangaza kuwa mchezo wa Ngao ya jamii kati ya Bingwa Mtetezi Yanga Sc na Mshindi wa Pili wa Ligi Kuu ya NBC Simba utapigwa September 16, 2025 katika uwanja wa Benjamin Mkapa. 

Mfumo wa mashindano ya Ngao ya Jamii umebadilika kutokana na marekebisho ya Kanuni yaliyopitishwa na kikao cha Kamati tendaji ya TFF.

Mashindano hayo yametoka kwenye mfumo wa mechi za mtoano kwa timu nne za juu kwemye msimamo wa Ligi Kuu hadi kupigwa kwa mtindo wa Bingwa ligi dhidi ya Bingwa wa Kombe la Shirikisho iwapo kama Bingwa zitakuwa timu mbili tofauti au Bingwa wa Makombe yote hayo mawili na mshindi wa nafasi ya pili kwenye Ligi.