Derby ya Kariakoo | Simba Vs Yanga kuchezwa Juni 15, 2025 kwa Mkapa

Bodi ya Ligi imefanya maboresho ya ratiba ya ligi kuu ya NBC ambapo mchezo namba 184 ulioota mbawa kati ya Yanga dhidi ya Simba uliopangwa hapo awali kupigwa Machi 8, 2025 sasa utapigwa Juni 18 na ligi hiyo itaisha June 22, 2025.

Mchezo huo wa Kiporo kati ya Yanga dhidi ya Simba utapigwa katika dimba la Benjamin Mkapa kuanzia saa 11:00 jioni.