Diamond Akanusha Kuongeza Mke.

SIMBA 🦁 @diamondplatnumz amekanusha uvumi unaosambaa mitandaoni ukidai kuwa ameongeza mke. ukurasa Wake Wa Instagram Ameandika: “Naona kuna misumari inapigiliwa kuwa Simba kaongeza mke. Hapana jamani, sijaongeza, msinipe ujasiri nisiokuwa nao.”

Aidha, Diamomd Ameweka Wazi kuwa video inayosambaa ikimuonesha akiwa ndani ya gari na msichana ni sehemu ya kazi yake mpya itakayotoka hivi karibuni.

Kwa mujibu wake, mwezi huu umepangwa kwa ajili ya “raha na burudani,” Kwa Ajili Ya Mashabiki Zake na siyo ugomvi wala maneno yanayohusu ndoa yake.