Diamond Ataka Taarifa Za Mbosso Zinazoendelea Zipuuzwe .

Nyota Wa Muziki Africa Na CEO Wa Label Ya @wcb_wasafi, SIMBA 🦁 @diamondplatnumz Ameibuka Kuzungumzia Kuhusu Taarifa Zilizosambaa Mtandaoni Za Msanii Wake @mbosso_ Kuondoka Katika Label Yake.

Diamond Kupitia IG Story Amesema Kwamba Amekuwa Na Mazungumzo Mazuri Na #Mbosso Na Hivyo Taarifa Zinazoendelea Mitandaoni Zipuuzwe Hadi Pale Yeye Na Mbosso Watakapotoa Tamko Rasmi .

“Tumekua na Mazungumzo Mazuri na @mbosso_ Namna ya kuanza Rasmi sasa Kusimamia Kazi zake na Tumekamilisha jambo letu Vizuri sana, Tafadhali Story yoyote inayozungumzwa kuhusu jambo hili la Mbosso. naomba zipuuzwe, Mpaka Mimi Binafsi na mbosso Tutakapotoa Tamko Rasmi” – Ameandika @diamondplatnumz

Je, Unadhani Jambo Gani Wamelikamilisha Vizuri ⁉️

✍️:#TRIGGAH (@officialtriggah_ )

AfricaIsWatching #WasafiDigital