Diamond Atoa Ngoma Mpya Na Focalistic, Inaitwa ‘Sasampa’.

SIMBA 🦁 @diamondplatnumz anaendelea kuthibitisha ukubwa wake katika soko la muziki Afrika baada ya kuachia wimbo wake mpya unaoitwa “Sasampa”, kama alivyoahidi kutoa nyimbo mfululizo mwezi huu wa Oktoba.

Baada Ya “Msumari” na “Nani”, Diamond sasa amewashirikisha wakali kutoka Afrika Kusini @focalistic 🇿🇦, @uncool_mc 🇿🇦, @silasafrica 🇿🇦, na @xduppy.012 🇿🇦 katika ngoma hii mpya Yenye ladha ya Amapiano Pamoja Na Bongo Fleva.

“Sasampa” ni neno lililopata umaarufu hivi karibuni, likiwa na maana ya hela au pesa, Na Hii inakuwa kolabo ya Pili (2) Kufanyika Kutoka Kwa Diamond Na Focalistic, Huku Kazi Yao Ya Kwanza Ikiwa Ni ‘Iyo’ Ya 2021.

Ngoma Hii “Sasampa” Inatajwa Kuwa miongoni mwa nyimbo Zitakazosumbua zaidi mwishoni mwa mwaka huu, ikizingatiwa ubora wa kolabo hiyo na uzito wa majina yaliyoshirikishwa.

JE, Umeisikiliza Mara Ngapi Ngoma Hii ⁉️