Spika wa Bunge la Tanzania Dkt Tulia Ackson amesema Serikali inatambua mchango wa vijana wasomi pamoja na kuheshimu mawazo chanya ambayo wamekuwa wakitoa katika muktadha wa kuijenga Tanzania.
Dkt Tulia ametoa kauli hiyo leo Jijini Dar es Salaam Juni 06, 2025 wakati wa mahafali ya Seneti ya Vyuo Vikuu kupitia UVCCM, ambapo pia alikabidhi vyeti kwa Wahitimu hao.
Akiwa hapo Dkt Tulia ametumia nafasi hiyo kuwahimiza vijana kujitokeza kwenye kushiriki kikamilifu kwenye uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba Kwa kujiandikisha kwenye Daftari la Wapiga na hatimae kupiga kura.
Leave a Reply