Don Jazzy Adai Inagharimu Tsh Milioni 200 – 700 Kumtengeneza Msanii Mpya Mavin.

Mmiliki wa lebo ya Mavin Records kutoka Nigeria, @donjazzy, kupitia mahojiano na Echo Podcast amefunguka kuhusu gharama halisi za kumsimamia msanii mpya ndani ya label yake.

Don Jazzy amedai kuwa inagharimu kati ya $100k – $300k (sawa na shilingi milioni 245 – 735 za Kitanzania) ili kumuandaa, kumtambulisha, kumfanyia promotion pamoja na mambo mengine muhimu ya kumjenga kisanaa.

Don Jazzy pia amesisitiza kuwa mafanikio ya msanii hayaji kirahisi, yanahitaji uwekezaji mkubwa, nidhamu na timu yenye maono. Kwa mujibu wake, wasanii wengi huona matokeo lakini wachache huelewa gharama na kazi kubwa iliyo nyuma ya pazia.