Drake Anunua Cheni Ya Marehemu Tupac.

Rapa #Drake amenunua Cheni Ya Marehemu 2Pac Yenye nembo ya “Death Row Records.” Cheni Hiyo iliyokuwa na maandishi ya “All Eyez on YOU” Imenunuliwa kutoka kwa Alexander Bitar, na Inachukuliwa Kama moja ya alama kubwa zaidi katika urithi wa 2Pac.

Cheni Ya Marehemu Tupac.

Cheni hii si ya kawaida kwani imewekwa maandishi ya kipekee “All Eyez on YOU” yaliyoongezwa na Suge Knight, mwanzilishi wa lebo ya Death Row, jambo linaloongeza thamani na uzito wa kihistoria wa kifaa hiki cha thamani. Kulingana na taarifa, Drake amenunua cheni hiyo kutoka kwa mtoza vitu vya thamani Alexander Bitar, ambaye anajulikana kwa kuwa na baadhi ya vitu vya kipekee zaidi duniani. Cheni hii inachukuliwa kama moja ya alama kubwa na zenye heshima katika urithi wa 2Pac, ikiwakilisha si tu maisha yake kama msanii, bali pia urithi aliouacha kwenye tasnia ya muziki wa Hip-Hop duniani. Kupatikana kwake mikononi mwa Drake kunathibitisha jinsi alivyokuwa msanii mwenye ushawishi mkubwa hadi leo.