Fainali Ya Kombe La Dunia 2026 Itakuwa Kama Superbowl.

Rais wa FIFA, Gianni Infantino, amethibitisha kuwa fainali ya Kombe la Dunia la 2026 itakuwa na Onesho la (Halftime Show) kwa mara ya kwanza katika historia ya mashindano hayo.

Onyesho hilo limepangwa kufanyika tarehe 19 Julai 2026 kwenye Uwanja wa MetLife huko New Jersey, likiandaliwa kwa ushirikiano na Global Citizen, huku Chris Martin na Phil Harvey wa Coldplay wakiratibu orodha ya wasanii watakaotumbuiza.

Wazo hili limehamasishwa na Onesho La Halftime Ya Super Bowl, FIFA inalenga kuongeza thamani ya burudani na kuvutia mashabiki wengi zaidi.