Baba wa msanii Asake, Mr Oduns Ameweka Wazi kuwa yeye na mwanaye Wamemaliza tofauti zao Na Sasa Wapo Katika Maelewano Mazuri. Akizungumza hivi karibuni, baba huyo alisema kuwa Asake ameanza kutimiza majukumu yake kama mtoto wake kwa kuhakikisha anapata mahitaji yake ya msingi na faraja ya kifamilia.
Kwa mujibu wa baba wa Asake, msanii huyo ameagiza watu wake watafute nyumba ya kununua kwa ajili yake katika eneo lililo karibu na kisiwa (Island). Tayari kwa saa 24 zilizopita, juhudi za kutafuta makazi hayo zimekuwa zikiendelea, jambo linaloashiria kwamba ameamua kumjali baba yake kwa vitendo.
Zaidi ya hilo, Asake pia amehakikisha kuwa atamtunza mtoto wake, Zeenat, kikamilifu na kugharamia mahitaji yote muhimu, ikiwa ni pamoja na bili za hospitali za baba yake.
Hata hivyo, baba wa Asake alifunguka kuhusu changamoto zilizokuwepo kabla ya maridhiano yao, akisema kuwa kilichokuwa kinamuumiza zaidi ni ukimya wa mwanaye kwa muda mrefu, hali iliyomfanya ahisi kama Asake hamjali. Alidai kuwa aliumizwa zaidi na jinsi mama yake Asake hakuwahi kumshinikiza au kumtia moyo kuulizia hali ya baba yake wala kushughulikia mahitaji yake.
Awali, baba wa Asake alikuwa ameibuka hadharani akidai kwamba hakuwa akipata msaada wowote kutoka kwa mwanaye, hali iliyozua mijadala mitandaoni. Lakini sasa, inaonekana hali imebadilika, na Asake ameanza kuchukua hatua kuhakikisha anatimiza wajibu wake kama mtoto.
Got a Questions?
Find us on Socials or Contact us and we’ll get back to you as soon as possible.