Hii hapa siri ya Arsenal kutwaa ubingwa wa EPL 2024/25

Gwiji wa soka barani Afrika, Yakubu Ayegbeni (42), ametoa ushauri kwa Arsenal kuhusu azma yao ya kushinda Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) msimu huu ambapo amesema kwamba Arsenal inahitaji kumsajili mshambuliaji mwenye uwezo wa hali ya juu ili kuweza kushindana na Liverpool, ambao wanaonekana kuwa washindani wakubwa.

“Msimu huu unaonekana kuwa na changamoto nyingi, ukiangalia jinsi Liverpool wanavyocheza, wanazidi kudondosha alama kidogo kidogo, ni fursa kwa Arsenal kuchangamkia hilo.

“Tumeona katika misimu michache iliyopita – mwaka jana, miaka miwili iliyopita, na miaka mitatu iliyopita, Arsenal wakiweka shinikizo kwa Manchester City, Hivi sasa, City haiko katika fomu bora.

“Kwa Arsenal (kushinda ligi), ni suala la kupata mshambuliaji. Mara tu watakapofanya hivyo, naamini wanaweza kuwatoa Liverpool kwenye mbio za ubingwa,” alisema Ayegbeni

The Gunners wameendelea na harakati zao za kuwania taji la Ligi Kuu ya England kwa ushindi mgumu wa mabao 2-1 dhidi ya Tottenham Hotspur kwenye Uwanja wa Emirates mchezo uliopigwa jana Jumatano, Januari 15, 2025.

#WasafiSports