Idadi ya Watalii yaongezeka nchini Tanzania

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chama amesema kuwa idadi ya watalii wa kimataifa imeongezeka kwa asilimia 132.1 kutoka watalii 922,692 Mwaka 2021 hadi watalii 2,141,895 Mwaka 2024.

Dkt. Pindi ameyasema hayo Leo mei 19,2025 Bungeni Jijini Dodoma wakati akiwasilisha Bajeti ya makadirio ya Mapato na matumizi ya Wizara Maliasili na Utalii ya mwaka wa fedha 2025/2026

Dkt. Pindi amesema kuwa Kwa idadi ya watalii wa ndani waliotembelea vivutio vya utalii imeongezeka kwa asilimia 307.9 kutoka watalii 788,933 Mwaka 2021 hadi kufikia watalii 3,218,352 mwaka 2024. Hatua hii imewezesha idadi ya watalii kufikia 5,360,247 sawa na asilimia 107.2 ya lengo la watalii
5,000,000

Aidha Dkt. Pindi amesema kuwa Kwa rekodi hizo, Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii (UN
Tourism), limeitaja Tanzania kuwa nchi iliyoongoza Afrika kwa mwaka 2024 kwa kuwa na ongezeko kubwa la watalii