Kesi ya Tundu Lissu yaahirishwa hadi Juni 2,2025

Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Tundu Lissu imeahirishwa hadi Juni 2, 2025 itakapotajwa tena katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,

Kesi hiyo ililetwa kwa ajili ya kutajwa, ambapo upande wa Jamhuri umeieleza Mahakama kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika.

Jamhuri imesema mpaka sana shauri hilo linaendelea na uchunguzi chini ya mamlaka za Kipolisi, na kwamba kwakuwa upelelezi haujakamilika hivyo wanaiomba Mahakama kuhairisha kesi husika kwa siku 14 zaidi, jambo ambalo limeonekana kupingwa vikali na Mawakili wa utetezi.

Jopo la Mawakili wa utetezi likiongozwa na Mawakili waandamizi Mpale Mpoki, Dkt. Rugemeleza Nshala na Peter waliwasilisha maombi kadhaa Mahakamani hapo, ambapo miongoni mwake wameiomba Mahakama kulazimisha upande wa Jamhuri ueleze nini hasa kinachokwamisha upelelezi kwa sababu mwanzo ilidaiwa Mahakamani hapo kuwa ushahidi wote kuhusiana na shauri hilo upo mtandaoni.