Rapa #JayZ Amefungua Kesi Ya Kuchafuliwa Dhidi Ya Mwanamke Aliyemtuhumu Kwa Kumbaka Mwaka 2000. Anadai Kuwa Ikiwa Mwanamke Huyo Tayari Alishakiri Kuwa Yalikuwa Ni Madai Ya Uwongo, Basi Hiyo Imemfanya Achukue Hatua Za Kisheria Dhidi Yake Na Wakili Wake “Buzbee” Kwa Kumchafua .
Kesi ya Mwanamke Huyu Ambaye Hakuwekwa Wazi Jina Lake (Jane Doe) ilifunguliwa awali dhidi ya ‘Diddy’ mwezi Oktoba 2024, ambapo alidai alipewa dawa za kulevya na kubakwa naye pamoja na mtu mwingine maarufu katika sherehe ya baada ya Tuzo za MTV Video Music Awards mwaka 2000, alipokuwa na umri wa miaka 13.
Katika malalamiko yaliyorekebishwa, yaliyowasilishwa Dec 2024, ‘Jay Z’ aliongezwa kama mshtakiwa na akashutumiwa kwa ubakaji. Hata Hivyo Jay Z, alikanusha vikali madai hayo, huku akimtaka mlalamikaji (Doe) kufungua kesi ya jinai na siyo ya madai kama alivyofanya endapo anaamini madai yake yana ukweli wowote dhidi yake.
Februari 15, 2025, mawakili wa mwanamke huyo walitoa taarifa ya mteja wao kufuta kesi dhidi ya mastaa hao huku uamuzi huo ukiwa na kipengele cha kutofunguliwa tena kesi hiyo katika siku za usoni, Wakidai Madai Hayo Hayakuwa Na Ukweli Wowote. Hivyo Jay-Z Ameamua Kumshtaki Mrembo Huyo Ikiwa Ni Wiki Moja Tu Kupita Tangu Aripotiwe Kumshtaki Wakili Wake.
Got a Questions?
Find us on Socials or Contact us and we’ll get back to you as soon as possible.