Jumba La Zamani La R. kelly Lauzwa Kwa Tsh. Bilioni 3.9/=.

Jumba La Zamani Ka Mwanamuziki Wa RnB ‘R.Kelly’ Limeuzwa Bei Ya Hasara Tofauti Na Bei Yake Ya Awali Iliyowekwa Sokoni $3.5M (Tsh Bilioni 8.5/=).

Nyumba hii ndiyo aliyokuwa akiishi na kurekodia nyimbo zake maarufu, lakini pia inadaiwa kuwa ndimo alikokuwa akifanya matukio yake ya unyanyasaji wa kingono kwa kila mwanamke aliyeingia.

Unaambiwa Changamoto Kubwa katika kuiuza nyumba hiyo ilikuwa ni bili ya kodi ya zaidi ya dola 120,000 iliyohusiana na mali hiyo. Nyumba Hiyo Ilikuwa Na: Vyumba 7 Vya Kulala, Mabafu 16, Gereji Yenye nafasi Ya Magari, Swimming Pool, Eneo L Kuchezea Mpira Wa kikapu (Basket Ball) N.k.

JE, Ungekuwa Na Kiasi Cha Hicho Cha Pesa Ungenunua Jumba La Staa Huyu ⁉️