Kampuni Ya Kusambaza Filamu Ya ‘Hulu’ imetangaza rasmi Kuiandaa Series Mpya ya “Prison Break”, ambapo itakuwa na wahusika wapya.
Kwa mujibu wa tovuti ya Deadline, Kazi Hii Inaandaliwa na Mtayarishaji Elgin James, ambaye ni mmoja wa waandaaji wa Mayans M.C., huku Paul Scheuring aliyeunda Prison Break ya awali akirudi kama mtayarishaji mkuu yani “executive producer”.
Hata Hivyo Bado Haijatangazwa Rasmi tarehe ya kuachiwa Kwa Series Hiyo Mpya na kama waigizaji wa awali watarudishwa katika Series hii mpya. Prison Break Ilianza kuachiwa rasmi Season 1 (2005) Na Ya Mwisho ambayo ni Season 5 (Revival) ilitoka 2017.
JE, Ulianza Kuifuatilia Series Hii Lini ⁉️
Got a Questions?
Find us on Socials or Contact us and we’ll get back to you as soon as possible.