Kamwe: tumewaalika simba Iftaar tunaomba wasitukimbie

Uongozi wa Yanga kupitia Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Ally Kamwe, leo, Machi 13, 2025 wameandaa Iftaar kwa wadau mbalimbali wa Soka nchini wakiwemo, viongozi wa mpira nchini, wasimamizi wa mpira, waandishi wa habari na timu za ligi kuu ikiwemo klabu ya Simba.

“Leo tutakuwa na Iftaar tumewaalika wadau mbalimbali wa soka nchini na wale wote ambao tunashirikiana nao kwenye mpira, tumewaalika ndugu zetu wa Simba, tunawaomba mje msitukimbie pale tunapokutana hakuna uwanja wa mpira hivyo msikimbie mje,” amesema Kamwe.