Kanye West Ampigia Simu Lil Durk Gerezani.

Tovuti Ya The Shade Room imepata video ya mazungumzo ya simu kati ya #KanyeWest na #LilDurk Ambaye Yupo gerezani Kwasasa Kwa Mashtaka Ya Mauaji Ya Kulipia (Murder For Hire). Katika mazungumzo hayo, Ye na Durk walikumbushiana wakati waliotumia pamoja Uraiani Huku Wakijadili Baadhi Ya Wasanii kama #DaveBlunts na wengine. Ye Amesikika Akimwambia Durk Kuwa Ametoka Kuongea Na Diddy Muda Si Mrefu Kabla Yake.

Chanzo kilicho karibu na Kanye kimesema kwamba Rapa Huyo Anapanga Kuyaunganisha Makundi Yote Ya Kihalifu (Gangs) Pamoja kwa mpango wa kutatua migogoro/ Kuzuia Mashambulizi Yanayohatarisha Maisha Na Kupelekea Vifo.

Chanzo hicho kimeongeza kuwa Ye na John Monopoly (Meneja Wa Kanye) wanakusudia kuwafikia viongozi wa magenge haya ili kuyashawishi Kuacha matumizi ya silaha na kupunguza mauaji. Magenge ambayo Ye anapanga Kuyafikia ni pamoja na: Gds, Bds, Breeds, 4s, MCs, Stones, LK, SD, 18th Str, Hoover’s, 8tre’s, 60’s, 20’s, Treetop, MOB, Pacoima Piru, Adams Family na mengineyo.