Kanye West Auza Eneo Lake Huko Wyoming Kwa Tsh. Bil. 34.4/=.

Tovuti ya TMZ imeripoti kwamba Kanye West ameipiga bei moja ya Ranchi zake zilizopo mjini Wyoming kwa ($14M) takribiani TSh. Bilioni 34.4/= ikiwa ni bei ileile ambayo alinunulia eneo hilo. Ye ameliuza eneo hilo tena kwa wamiliki waliomuuzia awali ‘Greg na Palm Flitner’.

Eneo ambalo Kanye Ameliuza Huko Wyoming

Eneo hilo lenye ukubwa wa ekari 4,000 lilikuwa miongoni mwa maeneo ambayo Kanye West aliyatumia kujichimbia na kufanya kazi zake ikiwemo utayarishaji wa album. Aliipa jina la West Lake Ranch au Yeezy Campus. Hili sio eneo pekee ambalo analimiki YE kwenye mji huo wa milima, kuna maeneo mengine mawili ambayo anayamiliki pia.