Kanye West Ndio Msanii Tajiri Zaidi Duniani 2025, Ana Utajiri Wa Tsh. Trilioni 7/=.

Kwa mujibu wa Erin Venture Services, Rapa Na Mfanyabiashara Kanye West (@ye), ameripotiwa kuwa mwanamuziki tajiri zaidi duniani mwaka 2025, akiwa na utajiri unaokadiriwa kufikia dola bilioni 2.77 Sawa Na Kiasi Cha Tsh. Trilioni 7/= .

Thamani hii kubwa inatokana zaidi na mafanikio ya kazi yake ya muziki pamoja na umiliki wake wa kipekee wa brand ya YEEZY, ambayo inaendelea kufanya vizuri sokoni.

Aidha, Kanye anapanua zaidi biashara Yake kwa kuzindua mavazi ya kike ya YEEZY, hatua inayoongeza ushawishi wake katika sekta ya mitindo.