Kendrick Lamar Avunja Rekodi Ya Michael Jackson Superbowl Halftime Show .

Shoo ya #KendrickLamar kwenye Super Bowl Halftime Show limeweka historia kama shoo ya laivu iliyotazamwa zaidi (watazamaji milioni 133.5) kwenye televisheni za Marekani tangu binadamu wa kwanza kutua mwezini mwaka 1969.

Kwa rekodi hii, Kendrick amempita hata #MichaelJackson, ambaye Halftime Show yake ya mwaka 1993 ilikuwa na watazamaji wengi zaidi kwa muda mrefu. Watamaji milioni 133.4 Wamarekani na bilioni 1.3 duniani.

Mbali na kuvutia mashabiki wa hip-hop, jukwaa lake la PlayStation liliongeza mvuto, likimfanya kufikiawatazamaji wengi zaidi hasa vijana na wapenzi wa video games.

Kwa mchanganyiko wa sanaa, teknolojia, na muziki, Kendrick Lamar ameandika historia mpya kwenye burudani za #SuperBowl