Mlinda mlango wa Timu ya Taifa ya soka ya Kenya, Patrick Matasi, yupo hatarini kukutana na mkono wa sheria baada ya kuvuja kwa video zilizorekodiwa kwa siri hivi karibuni, zikimuonesha akifanya mazungumzo ya kupanga matokeo ya mechi ya Ligi Kuu Kenya (KPL).
Video hizo zinamuonesha kipa huyo wa zamani wa Police FC na sasa akiitumikia klabu ya Kakamega Homeboyz akiwa ndani ya gari (siti ya nyuma upande wa kulia) akijadili mpango wa kuseti matokeo, akiwa hana ufahamu kama anarekodiwa na mtu aliyekaa upande wake wa kushoto ingawa bado haijajulikana ni lini hasa tukio hilo lilifanyika.
Matasi nchini Kenya anatambulika kama mmoja wa makipa bora mno wanaokipiga nchini humo lakini, kiwango chake katika mechi muhimu za hivi karibuni kimeibua maswali mengi miongoni mwa mashabiki hao wakiwemo wale wa Harambee Stars, ambao wamekuwa wakilalamikia uzembe wake uliowahi kuigharimu timu hiyo ya Taifa.
Licha ya uzoefu pamoja na ubora alionao kipa huyo, vyote hivyo havikutosha kuzuia minong’ono ya aidha kushuka kiwango au sababu nyinginezo ikiwemo kupanga matokeo na kwa mujibu wa video hizo ni wazi kilichokuwa kinasemwa juu yake huenda kikawa na ukweli.
Got a Questions?
Find us on Socials or Contact us and we’ll get back to you as soon as possible.