Kocha wa Bayern Munich, Vincent Kompany, ameongeza rasmi mkataba wake na klabu hiyo ya Bundesliga hadi Juni 2029.
Kompany, ambaye alijiunga na Bayern Munich mwaka 2024 akitokea Burnley, amekuwa akipambana kukijenga kikosi hicho.
Uongozi wa Bayern umeonesha imani kubwa kwake kutokana na maendeleo ya timu chini ya uongozi wake.
Kupitia taarifa rasmi ya klabu, Bayern Munich imesema: “Tuna furaha kutangaza kwamba Vincent Kompany ameongeza mkataba wake hadi Juni 2029. Ameonyesha dira na falsafa thabiti ya soka ambayo inaendana na malengo ya klabu.”
Kwa upande wake, Kompany alionyesha furaha yake akisema: “Ni heshima kubwa kuendelea na safari hii na Bayern Munich. Nimejifunza mengi katika muda mfupi, na malengo yetu ni kuhakikisha tunarejesha hadhi ya Bayern kuwa kinara barani Ulaya.”
Mkataba huu mpya unathibitisha dhamira ya Bayern Munich ya kumpa Kompany muda wa kujenga kikosi imara chenye mwelekeo wa muda mrefu.
Got a Questions?
Find us on Socials or Contact us and we’ll get back to you as soon as possible.