Lamine aipa Liverpool ubingwa wa UCL 2024/25

Mshambuliaji wa Barcelona, Lamine Yamal (17), amewapa nafasi kubwa Liverpool ya kushinda ubingwa wa ligi ya mabingwa msimu huu wa 2024/2025.

“Nahisi Liverpool ndo wana nafasi kubwa ya kushinda ubingwa kuliko sisi, wao ndo wamemaliza nafasi ya kwanza, tutashindana ili tuweze kuwa mabingwa hatutabaki nyuma” amesema Yamal

Barcelona walimaliza nafasi ya pili nyuma ya Liverpool kwenye hatua ya makundi na kupata tiketi ya moja kwa moja  kwenda hatua ya kumi na sita bora.