Lavalava Atoa Ep Yake Mpya

Msanii wa Bongo Fleva, Lava Lava, amerudi rasmi kwenye anga ya muziki kwa kishindo baada ya kuachia EP yake mpya iitwayo Time. Kazi hii ina jumla ya nyimbo tano, ikionesha mwelekeo mpya wa kisanii na ubunifu wake baada ya kipindi cha ukimya.

Time ni kazi yake ya kwanza mkubwa tangu kuondoka kwenye lebo ya WCB Wasafi, hatua inayotazamwa kama mwanzo wa sura mpya katika safari yake ya muziki. Kupitia EP hii, Lava Lava anawaletea mashabiki wake mchanganyiko wa midundo ya Bongo Fleva na ladha za kimataifa, akithibitisha bado ana nafasi kubwa kwenye tasnia ya muziki wa Afrika Mashariki.