Lil Durk Adai Akitoka Jela Ataongoza Kwa Mfano.

Lil Durk Ametoa Ujumbe Huu Katika Siku Ya Kumbukizi Ya Kuzaliwa Kwake Oct 19 Akitimiza Umri Wa Miaka 33. Rapa Lil Durk Amesikika Akiongea Na Simu Jela Akisema Kwamba;

“Niko vizuri zaidi,. Kila mtu anapewa nafasi ya pili… Nikitoka hapa, nitaongoza kwa mfano” – Durk Akidai Kuwa Amejifunza na anahisi kwamba amebadilika, Hivyo Anataka kutumia nafasi hiyo mpya kuonyesha mabadiliko kupitia vitendo, na si maneno (Kuongoza Kwa Mfano).

Lil Durk Alikamatwa Oct 2024 Kwa Mashtaka Ya Mauaji Ya Kulipia (Murder For Hire) Huko Broward, Florida. Durk anashutumiwa kwa kupanga mauaji ya Saviay’a “Lul Pab” Robinson, binamu wa rapper Quando Rondo, katika shambulio lililotokea Los Angeles mwaka 2022. Shambulio hilo linadaiwa kuwa ni kisa cha kulipiza kisasi kwa kifo cha King Von mwaka 2020.

Hivyo Durk anashikiliwa bila dhamana na anakabiliwa na mashtaka ya njama ya mauaji, Kutumia Silaha Bila Kibali, na mauaji ya Kulipia (Murder For Hire). Kesi Yake Inatarajiwa Kusikilizwa Januari 20, 2026.