Lil Wayne Atangaza Tarehe Ya Kuachia Album Yake Mpya ‘The Carter Vi’

Lil Wayne kuachia album yake “Tha Carter VI” Juni 6, 2025. Taarifa Hii Imetolewa na rapa Huyo Kupitia X (Twitter) akisema Ataachia album hiyo Ifikapo Juni 6 Mwaka Huu kwenye majukwaa ya kusikiliza na kupakua muziki mtandaoni.

Lil Wayne Aliwahi Kuulizwa na Variety, kuhusu album aipendayo kwenye mtiririko wa Tha Carter. Lil Wayne alijibu kwamba anaipenda Tha Carter VI; “My favourite Carter album is the next one”

Ni miaka 7 Sasa imepita tangu Lil Wayne aidondoshe Tha Carter V (5), album ambayo ilitoka Septemba 28, 2018 ikiwa na jumla ya ngoma 23. Album Hii ilitoka kwa Mbinde mara baada ya Lil Wayne kuishikilia kwa takribani miaka 8 kutokana na kukosekana kwa maelewano kati yake na Birdman.