Lissu awaasa Bavicha Kuchagua Viongozi Majasiri

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara Tundu Antiphas Lissu amewataka wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Baraza la Vijana la Chama hicho kuchagua viongozi wenye ujasiri watakaosaidia kufikia malengo ya Baraza Hilo.

Tundu Lissu ambaye pia ni mgombea wa nafasi ya uenyekiti Taifa ametoa nasaha hizo wakati akizungumza kwenye mkutano mkuu wa BAVICHA unaoendelea jijini Dar Es Salaam.