Mahakama yamzuia Tory Lanez Kumkaribia Megan Thee Stallion

Hakimu ameidhinisha amri ya miaka mitano ya kumzuia Tory Lanez kumkaribia Megan Thee Stallion.

Megan alitoa shahidi kupitia video wakati wa kusikilizwa kwa kesi ya amri ya kumzuia, akieleza hofu yake kuhusu kile kinachoweza kutokea Tory akiachiliwa kutoka gerezani.

“Nahisi huenda atanipiga risasi tena, na huenda safari hii nisipone,” alisema Megan.

Tory Lanez hatakuwa na haki ya kuomba parole hadi Septemba 2029. Amri hii ya kumzuia, iliyotolewa na Hakimu Bloom, itadumu kwa miaka mitano, hadi Januari 9, 2030.