Man United bado hawajakata tamaa kwenye dili la Baleba

Klabu ya Manchester United imepanga kuendelea na mazungumzo mapya katika siku chache zijazo kwa ajili ya kumsajili kiungo wa Brighton & Hove Albion, Carlos Baleba. 

Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zinaeleza kuwa United inaamini mchezaji huyo kutoka Cameroon ana hamu kubwa ya kujiunga nao, na kwamba makubaliano binafsi ya mkataba hayataweka kizuizi katika mpango huo.

Hata hivyo, upande wa Brighton unaonekana kuifanya dili hiyo kuwa gumu kutokana na thamani kubwa wanayomuwekea Baleba, ambaye amekuwa mchezaji muhimu katika kikosi chao. 

Manchester United inatarajiwa kuendeleza mawasiliano na viongozi wa Brighton ili kutafuta mwafaka, licha ya changamoto hizo.

Baleba, ambaye amekuwa akivutia macho ya vilabu vikubwa barani Ulaya kutokana na uwezo wake wa kiufundi na nguvu zake katikati ya uwanja, anatajwa na kocha wa United kama sehemu ya mpango wa kuimarisha safu ya kiungo kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu England.

Endapo makubaliano yatapatikana, usajili wa Baleba unaweza kuwa moja ya dili kubwa kwa Manchester United katika dirisha hili la usajili.