Martin Classic Atoa Wimbo Mpya Akimshirikisha Mpenzi Wake Maggie Bushiri .

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Martin Classic, ameachia wimbo wake mpya unaoitwa “Milele”, ambapo amemshirikisha mwimbaji mwenye sauti ya kipekee, Maggie Bushiri. Ngoma hii inakuja kama muendelezo wa kazi bora kutoka kwa msanii huyo, ambaye amekuwa akijizolea umaarufu kutokana na ladha yake ya kipekee kwenye muziki.

Wimbo wa “Milele” unazungumzia mapenzi ya dhati na ahadi ya kupendana milele, ukiwa na midundo laini inayochanganya ladha ya Afrobeat na Bongo Fleva. Martin Classic na Maggie Bushiri wameonyesha uwezo wao mkubwa wa kushirikiana, wakileta vionjo vya kipekee vinavyovutia mashabiki wa muziki wa mapenzi.

Hii si mara ya kwanza kwa wasanii hawa kushirikiana, kwani wamekuwa wakifanya kazi pamoja katika nyimbo kama “Sale” wakimshirikisha Aslay, pamoja na vibao vingine vilivyopata mapokezi mazuri.

Kwa sasa, mashabiki wanaweza kusikiliza wimbo “Milele” kwenye majukwaa mbalimbali ya muziki, huku Tayari video rasmi ya wimbo huu Umeshatoka Kwenye Youtube Channel Ya Martin Classic. Hata Hivyo Martin Classic ameahidi kuendelea kutoa burudani kwa mashabiki wake kupitia Kazi Zinazokuja.

https://youtu.be/xiqRbFeCCi0?si=9sYVDw6CtBhL8CeQ