Jeshi la Polisi mkoani Pwani linamshikilia Tanganyika Masele (32) kwa tuhuma ya mauaji ya mke wake na mtoto wao mdogo ambapo aliwakata shingoni kwa kitu chenye ncha kali na miili yao kutupwa karibu na bwawa la maji.
Tukio hili la kusikitisha lilitokea Februari 17, katika Kitongoji cha Buduge, Kata ya Marui, Wilaya ya Kisarawe ambapo Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Salim Morcase, amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo.
Morcase amewataja marehemu ni , Gumba Kulwa, (27) na mtoto wake Masele Tanganyika na wote walikutwa wamekatwa shingoni kwa kitu chenye ncha kali na miili yao kutupwa karibu na bwawa la maji jirani na nyumbani kwao.
Amesema uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa chanzo cha tukio hilo ni wivu wa mapenzi na mara kwa mara alikuwa akitishia kumuua mkewe na mtoto wake.
Baada ya tukio hilo, Polisi walimkamata mtuhumiwa kwa ushirikiano na viongozi wa kijiji na wananchi.
Kamanda Morcase ametoa wito kwa jamii kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi na kufuata sheria za nchi.
Mauaji Pwani: Tanganyika amuua mkewe na Mtoto kisa Wivu wa mapenzi

Leave a Reply