Mlinda mlango chipukizi Cheikh Touré (18) kutoka Senegal ameuawa kikatili nchini Ghana baada ya kutekwa na kundi la watu wasiojulikana waliokuwa wakidai fidia kutoka kwa familia yake.
Kwa mujibu wa taarifa zilizothibitishwa na Wizara ya Ushirikiano wa Afrika na Masuala ya Nje ya Senegal, Touré alisafiri kuelekea Ghana kwa nia ya kushiriki majaribio ya soka (trials) yaliyodaiwa kupangwa na mawakala wa uongo waliomvutia kwa ahadi ya kupata nafasi katika klabu.
Hata hivyo, safari hiyo iligeuka kuwa ya mauti baada ya kijana huyo kutekwa nyara muda mfupi baada ya kuwasili nchini humo.
Watekaji walidai kiasi cha fedha kutoka kwa familia yake ili kumuachia huru, lakini juhudi za kukusanya fedha hizo zilishindikana. Siku chache baadaye, mwili wa Cheikh Touré ulipatikana katika mji wa Kumasi, Mkoa wa Ashanti, Ghana.
Mamlaka za Ghana kwa sasa zimeanzisha uchunguzi wa kina kubaini waliotekeleza uhalifu huo, huku Ubalozi wa Senegal nchini Ghana ukishirikiana nao kuratibu taratibu za usafirishaji wa mwili wake kurudi nyumbani kwa maziko.
Serikali ya Senegal imetoa wito wa tahadhari kwa wachezaji na familia zao, ikisisitiza umuhimu wa kuthibitisha uhalali wa mawakala au mialiko ya michezo kabla ya kusafiri nje ya nchi.
Got a Questions?
Find us on Socials or Contact us and we’ll get back to you as soon as possible.