Mnyika aeleza kwanini hakwenda kusaini kanuni za maadili

Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA John Mnyika amesema kilichomfanya kutokwenda kusaini kanuni za maadili ya Uchaguzi Mkuu 2025 ni kutokana na madhila wanayodai kuyapitia katika chaguzi zilizopita ikiwemo uchaguzi mkuu wa 2020 na wa serikali za mitaa wa 2024.

Mnyika ameeleza hayo wakati akizungumza na wananchi wa wilaya ya Babati mkoani Mnayara kwenye ziara ya Kichama yenye kampeni ya No reforms No election inayoendeleakanda ya Kaskazini.

Amesema wao kama CHADEMA walipendekeza kufanyika kwa mabadiliko ya sheria za uchaguzi ili kutoa fursa za vyama kushiriki kwa uhuru.