Unaambiwa Mmoja Kati Ya Washukiwa Wa Wizi Wa Vito Vya Thamani Ya $10M+ (Tsh Bilioni 26+) Vya Kim Kardashian Amefariki Dunia Ghafla Kabla Ya Kesi Kuanza Jumatatu Hii. Kwa Mujibu Wa TMZ.
Mtuhumiwa Huyo ‘Marceau Baum-Gertner’ Alifariki Dunia March 6 Huku Sababu Ya Kifo Chake Bado Haijawekwa Wazi. Kwa Mujibu Wa Ripoti Mbalimbali Kulikuwa Na Uwezekano Mkubwa Wa Mtuhumiwa Huyu Kutaja Majina Ya Waliohusika Na Mchongo Mzima Wa Wizi Ili Apunguziwe Adhabu Ya Kifungo.
Kumbuka 2016 Kim Aliripotiwa Kuporwa vito vya thamani ya zaidi ya Dola za Marekani Milioni 10 na watu waliokuwa na silaha Za Moto Wakati akiwa amepumzika Kwenye Moja Ya Hotel Mjini Paris, Ufaransa Alipoenda Kwa Ajili Ya ‘Fashion Week’.
Kim aliibiwa vito hivyo baada ya kuvamiwa Hotelini, Ambapo watekaji walimfunga kamba kisha Kumfungia bafuni na baada ya Kukamilisha Zoezi Lao, walitoweka eneo la tukio.
Sasa Kim Kardashian anaripotiwa kuwa atatoa ushahidi dhidi ya genge la Baum-Gertner la mjini Paris, linalodaiwa kupanga wizi wa mali yenye thamani ya dola milioni 10+.
Got a Questions?
Find us on Socials or Contact us and we’ll get back to you as soon as possible.