Mwanasayansi wa Ufaransa Aliyevumbua Dawa ya Utoaji Mimba Afariki Dunia

Mwanasayansi maarufu kutoka Ufaransa, Étienne-Émile Baulieu, aliyegundua dawa ya kutoa mimba (mifepristone), amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 98 nyumbani kwake mjini Paris.

Baulieu alipata umaarufu mkubwa duniani kutokana na kazi yake ya kisayansi iliyopelekea kupatikana kwa dawa ya RU-486, inayojulikana pia kama mifepristone, ambayo imewapa mamilioni ya wanawake ulimwenguni kote njia mbadala salama na ya bei nafuu ya utoaji mimba kwa upasuaji.

Kwa mujibu wa mke wake, Simone Harari Baulieu, alieleza kuwa Utafiti wake uliongozwa na dhamira yake ya maendeleo kupitia sayansi, kujitolea kwake kuwapa uhuru wanawake na hamu yake ya kumuwezesha kila mtu kuishi maisha bora na marefu.””