Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameikabidhi familia ya aliyekuwa muigizaji mashuhuri wa ucheshi, Amri Athuman, maarufu kama Mzee Majuto, tuzo ya heshima ikiwa imeambatana na hundi ya shilingi milioni 30.
Heshima hiyo imetolewa katika hafla ya Tuzo za Ucheshi Tanzania (Cheka na Samia) zinazofanyika leo, Februari 22, 2025, katika ukumbi wa The Superdome, Masaki, jijini Dar es Salaam.

Tuzo hiyo ni ishara ya kutambua mchango mkubwa wa Mzee Majuto katika tasnia ya vichekesho nchini, ambapo alihusika katika kuinua vipaji na kuburudisha Watanzania kwa miongo mingi kupitia filamu na michezo ya kuigiza.

Katika hafla hiyo, viongozi mbalimbali wa serikali, wasanii wa vichekesho, na wadau wa tasnia ya burudani wamehudhuria kusherehekea mafanikio ya tasnia ya uchekeshaji Tanzania.
Leave a Reply