Nandy Atangaza Kuachia Album Mpya Novemba Mwaka Huu, Atoa Wimbo Mpya ‘Tonge Nyama’

Msanii Wa Muziki Wa Bongo Fleva Nchini @officialnandy Ametangaza Ujio Wa Album Yake Mpya Itakayotoka Novemba Mwaka Huu 2025. 

Kupitia Ukurasa Wake Wa Instagram (IG Story) Amethibitisha Taarifa Hiyo Kwa Kuandika; 

“Mashabiki zangu comment zenu naziona kuhusu album ok niwaambie tu album itatoka mwez 11 kwa sababu za kimsingi kabisa! Tunamalizia some colabo na maandalizi mazima ya album yenyewe, tungependa kutoa burudani kipindi tulivu na rahisi kwetu thank you tuendelee ku enjoy mziki mzuri.” – Nandy 

Nandy Kupitia Ukurusa Wake Wa Instagram

Kwasasa Tayari Ameachia Video Ya Ngoma Yake Mpya Iitwayo ‘Tonge Nyama’, Hivyo Huenda Wimbo Huu Ukakutana Nao Katika Album Yake Hiyo Mpya.