Napoli kwenye hatua za mwisho kumnasa Hojlund

Klabu ya Napoli ipo kwenye hatua za mwisho kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa Denmark, Rasmus Højlund, akitokea Manchester United.

Kwa mujibu wa taarifa, pande zote zipo kwenye mazungumzo ya mwisho huku Napoli ikionyesha kujiamini kwamba dili hilo litakamilika muda si mrefu. 

Mpango uliopo ni mkopo wenye kipengele cha kumnunua ambacho kitapewa masharti ya lazima, kwa ada inayokaribia euro milioni 45.

Endapo makubaliano yatakamilika, Højlund atasaini mkataba wa muda mrefu utakaomuweka Italia hadi mwezi Juni mwaka 2030. 

Kitu pekee kilichosalia kwa sasa ni makubaliano ya mwisho kuhusu masharti ya kuondoka kwake Manchester United.

Iwapo dili hili litakamilika, litakuwa hatua kubwa kwa Napoli kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji wao kwa msimu ujao.