Muigizaji na Mwanamitindo, Nelly Kamwelu amemuomba msamaha mama yake na kukiri kuwa mapenzi yalimtawala akili kufikia hatua ya kutosikiliza ushauri wake mpaka kufikwa na majanga ya kupewa kipigo na aliyekuwa mpenzi wake
Akizungumza kupitia Mashamsham ya Wasafi FM, Nelly Kamwelu amesema kuwa kwa sasa anasikiliza nini mama yake anamuambia kwani madhara ya kutosikiliza ameyashuhudia kwa macho yake
Wiki kadhaa zilizopita, muigizaji huyo alijikuta akiuguza majeraha mwili mzima baada ya kupokea kipigo kikali kutoka kwa aliyekuwa mpenzi wake huku chanzo kikitajwa kuwa ni wivu wa mapenzi
Mbali na hayo, pia Nelly Kamwelu ameeleza namna familia ya aliyekuwa mpenzi wake ilivyomtorosha kijana wao kwa kumsafirisha ingalikuwa bado kuna kesi polisi
Nelly amesema amesamehe yote aliyofanyiwa na mwanaume huyo ila ameweka wazi kuwa hawezi kurudiana naye kamwe

Leave a Reply