Offset Aomba Kulea Watoto Pamoja Na Cardi B

Licha ya kutengana kwao kwa hali isiyo ya amani, #Offset sasa anataka mgawanyo sawa wa malezi ya watoto wake na #CardiB. Kwa mujibu wa ripoti ya TMZ iliyotolewa ljumaa (Februari 28), nyaraka mpya za mahakama zinaonyesha kuwa Offset amewasilisha ombi la kuwa na haki sawa ya kisheria juu ya malezi ya watoto wao watatu.

Hata hivyo, Offset anapendekeza kwamba makazi ya Cardi B yawe makazi maalum kwa watoto hao, huku akisisitiza kuwa anahitaji muda wa kutosha kuwa nao. Mbali na hilo, Offset pia ameomba mali wanazomiliki kwa pamoja igawanywe kwa usawa na kila mmoja wao ajitegemee kwa gharama za mawakili wake.

Ikiwa maombi haya yatakubaliwa, itakuwa hatua rasmi ya kumaliza mgogoro wa talaka yao uliojaa malumbano ya maneno na majibizano hadharani tangu Cardi B alipowasilisha ombi la talaka Agosti 2024.