Unakumbuka mahojiano ya msanii @omah_lay mwaka jana aliyofanya na podcast moja nchini Marekani, ambapo alidai album yake ilichelewa kutoka kwa sababu aliibiwa idea na sound mpya aliyotaka kuitambulisha kwa mashabiki?
Katika mahojiano hayo, Omah Lay alisema aliibiwa wazo hilo na msanii mwenzake aliyemuamini sana.
Sasa, leo hii, Omah Lay ametumia akaunti yake nyingine ya siri Ya Instagram kuvujisha screenshots za Chats Zake na msanii huyo ambaye ni #Rema. Katika Chats Hizo, Zinaonesha Omah Lay Alivyo-Share Wazo La Sound Yake Mpya Kwa Rema Na Jinsi Walivyotaka kuitambulisha kwenye muziki. Hivyo Anamtuhumu kwa kuiba wazo hilo na kulibadilisha kuwa sehemu ya album yake Heis.


Omah Alidai kwamba baada ya kumshirikisha Rema wazo hilo, Rema alitoa album yenye Wazo Lilelile, jambo lililomlazimu Omah Lay kurekodi upya album yake yote. Sound Inayodaiwa Ni Ile Ya ‘Ozeba’.
Got a Questions?
Find us on Socials or Contact us and we’ll get back to you as soon as possible.