Vatican imetangaza kifo cha Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis kilichotokea leo Jumatatu ya Pasaka, Aprili 21, 2025, katika makazi yake ya Casa Santa Marta
Papa Francis amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 88, wiki chache baada ya kuruhusiwa kutoka hospitali mjini Rome alikokuwa akipatiwa matibabu kutokana na ugonjwa wa nimonia uliokuwa umeshambulia mapafu yote mawili.
Papa Francis, ambaye alichaguliwa kuwa kiongozi wa Kanisa Katoliki mwaka 2013, alikuwa Papa wa kwanza kutoka Amerika ya Kusini na mmoja wa mapapa wa umri mkubwa zaidi kuwahi kuliongoza Kanisa hilo.
Taarifa zaidi Zitakujia, Endelea kufuatilia kurasa zetu
Leave a Reply