Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo, amekiahiza Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kuhakikisha kinashirikisha na sekta binafsi katika kuendeleza utafiti na uvumbuzi nchini, huku serikali ikiwa na nia ya kutoa angalau asilimia moja ya pato la taifa ili kuelendeleza tafiti hizo.
Profesa Kitila ametoa wito huo Juni 9, 2025 jijini Dar es Slaam, katika Ufunguzi wa Maonyesho ya 10 ya Utafiti na Uvumbizi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa mwaka 2025, ambapo pia amevitaka vyuo vyote nchini kuendelea kusimamia misingi ya taaluma ya vyuo vikuu, ikiwa ni pamoja na uhuru wa kitaaluma.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam anayeshughulika na Masuala ya Utafiti Profesa Nelson Boniphace, akizungumza katika maonyesho hayo, amesema kuwa matumizi ya teknolojia za kidigitali katika kuhakikisha uharakishwaji wa ubunifu na utafiti, ni ajenda inayopewa kipaumbele kwa mwaka 2025, ikiwa ni hatua muhimu ya kutatua matatizo yanayoikabili Tanzania kwenye sekta ya utafiti na Uvumbuzi.
Joshua Sumbuka ni Mwanafunzi wa mwaka wanne kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam katika shule ya madini na elimu miamba, anazungumzia namna ambavyo akili Mnemba ilivyo muhimu katika mapinduzi ya kiteknolojia, akiwa miongoni mwa vijana waliojitokeza kwenye maonyesho hayo, kwa upande wa teknolojia ya uchenjuani dhahabu, huku Amideus Athanas kutoka Idara ya Kilimo, na Dkt. Charles Domisian kutoka kitivo cha kilimo na teknolojia za chakula, wakieleza kuwa upo umuhimu wa tafiti katika sekta mbalimbali, kupitia teknolojia hiyo.
Leave a Reply